Katibu mkuu UN apongeza makubaliano ya serikali ya Afghanistan na kundi la Taliban kuharakisha mazungumzo
2021-07-20 09:09:40| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza makubaliano kati ya serikali ya Afghanistan na kundi la Taliban kuharakisha mazungumzo ya amani.

Bw. Guterres amesema ametiwa moyo na taarifa ya pamoja iliyotolewa huko Doha, Qatar, ambayo imeeleza kuwa pande mbili zimekubali kuharakisha mawasiliano ya ngazi ya juu kati yao, ili kupata “utatuzi wa mgogoro wa haki kwa wakati”.

Bw. Guterres amesema hayo kupitia taarifa ya pamoja iliyotolewa na tume ya kidiplomasia ya nchi 15, jumuiya ya NATO na Umoja wa Ulaya kwa Afghanistan, ikitoa wito kumaliza mabavu na kuwa na usimamishaji wa vita wa kudumu na wa pande zote, pamoja na mazungumzo ya amani yenye maana.