Umoja wa Afrika wasisitiza uwepo wa mpango wa ufufuaji baada ya COVID-19 unaohimili mabadiliko ya tabia nchi
2021-07-20 08:26:02| CRI

Umoja wa Afrika umesisitiza haja ya kuwepo kwa mpango wa ufufuaji baada ya janga la COVID-19 utakaohimili mabadiliko ya tabia nchi.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imesema janga la COVID-19 linaloendelea limesababisha kudorora vibaya kwa uchumi kuwahi kuonekana kwa karibu karne moja, na madhara yake kwa Afrika yamekuwa makubwa.

Umoja huo umesema kukosekana kwa usalama wa chakula na mzigo wa madeni vimekuwa vikiongezeka, na maendeleo yaliyopatikana kwa ngazi ngumu yanapotea.

Wakati huo huo wataalam wa afya wa nchi za Afrika wametaka uwekezaji zaidi uwepo kwenye utafiti wa ndani wa chanjo salama na yenye ufanisi, ambayo itakuwa hatua muhimu ya kuimarisha mapambano dhidi ya COVID-19 barani Afrika.

Mkuu wa kundi la kimataifa la ushauri wa mambo ya afya (Amref Health Africa) lenye makao yake mjini Nairobi Bw. Githinji Gitahi, amezitaka serikali za nchi za Afrika kuongeza bajeti za utafiti wa chanjo ya COVID-19, wakati zikijadiliana na makampuni ya nchi za nje kuhusu haki miliki za kutengeneza chanjo hiyo.