China yaripoti matokeo yaliyopatikana kwenye utafiti wa anga ya juu
2021-07-21 09:13:32| CRI

Akademia ya Sayansi ya China imetangaza mafanikio yaliyopatikana kwenye utafiti wake wa anga ya juu, ikiwa ni pamoja na utambuzi wa mawimbi ya nguvu ya uvutano, majaribio ya uvutano mdogo, na ufuatiliaji wa mlipuko kwenye tundu jeusi.

Akademia hiyo imesema satellite ya Taiji-1 ambayo ni satellite ya kwanza ya China kutafiti teknolojia muhimu za utambuzi wa mawimbi ya nguvu ya uvutano, imekamilisha majukumu yake.

Satellite nyingine ya kupima nguvu ndogo ya uvutano SJ-10, nayo pia imefanikiwa kutafiti maendeleo ya seli kwa mamalia, na darubini ya Insight ambayo nayo kwa mara ya kwanza imeweza kupata picha nzuri ya mlipuko wa tundu jeusi.

Satellite hizo tatu zilitengenezwa na Akademia hiyo ikiwa ni sehemu ya mradi wa utafiti wa anga ya juu.