Rais Xi Jinping wa China atoa maagizo muhimu kufuatia mvua kubwa kuukumba mkoa wa Henan
2021-07-21 13:50:28| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa maagizo muhimu kufuatia mvua kubwa kuukumba mkoa wa Henan na kusabibisha vifo vya watu na hasara kubwa za mali.

Rais Xi amewataka maofisa wa ngazi mbalimbali watoe kipaumbele katika kulinda usalama wa maisha na mali za wananchi, kuwashughulikia kwa hatua mwafaka watu walioathirika na maafa na kupunguza kadri iwezekanavyo vifo vya watu na hasara za mali. Pia ameviamuru vikosi vya jeshi na polisi kushirikiana na serikali ya mitaa katika kazi ya kuokoa maafa.