Waziri Mkuu wa China asisitiza umuhimu wa kuendeleza utafiti wa kimsingi
2021-07-21 09:14:12| CRI

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa mwito wa kuhimiza mageuzi ya mapitio ya miradi ya utafiti wa kisayansi na utaratibu wa uchambuzi ili kuhimiza watafiti kujikita kwenye utafiti wa kimsingi.

Akiongea kwenye kongamano la mfuko wa sayansi za asili la taifa NSFC, ambalo mwaka huu linaadhimisha miaka 35, Bw. Li amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kulikuwa ni hatua muhimu katika upangaji wa raslimali za sayansi na teknolojia, kutoka mfumo ulioratibiwa na serikali hadi mfumo unaoratibiwa kwa ushindani.

Bw. Li amekumbusha kuwa changamoto nyingi za kiteknolojia kwenye viwanda vingi, inatokana na udhaifu kwenye uvumbuzi wa asili, na kusema utafiti wa kimsingi ni hatua muhimu ya kuhimiza utafiti wa asili, sayansi na teknolojia, na maendeleo ya viwanda.

Pia ametoa mwito wa kuhimiza ushirikiano wa kimataifa kwenye utafiti wa kisayansi.