Tetemeko lenye nguvu ya 7 kwenye kipimo cha Richter latokea kwenye mpaka wa Costa Rica na Panama
2021-07-22 09:10:14| CRI

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7 kwenye kipimo cha Richter limetokea kwenye eneo la mpaka kati ya Costa Rica na Panama saa tisa na robo usiku kwa saa za huko.

Kiini cha tetemeko hilo kimetajwa kuwa kilometa 113 kusini mwa mji wa Punta Burica, Panama kwenye kina cha kilometa 10 kwenye bahari ya Psifiki.

Nchini Costa Rica tetemeko hilo lilisababisha milio ya tahadhari karibu nchi nzima, lakini ni katika mji mkuu San Jose na mingine mikubwa ndiko wakazi waliripoti kuanguka kwa vitu. Hadi sasa hakuna ripoti kuhusu uharibifu mkubwa kwa majengo au watu kujeruhiwa.

Kamati ya taifa ya mambo ya dharura imeondoa uwezekano wa kutokea kwa hatari ya tsunami.