Kundi la Taliban ladhibiti nusu ya maeneo ya kati ya wilaya nchini Afghanistan
2021-07-22 09:42:02| cri

Mnadhimu mkuu wa jeshi la Marekani Jenerali Mark Milley amesema wapiganaji wa kundi la Taliban wamedhibiti nusu ya maeneo ya kati ya wilaya zote 419 nchini Afghanistan.

Jenerali Milley amesema inaonekana kundi la Taliban linaendelea na mwelekeo huo wa kimkakati japo hadi sasa halijateka mji mkuu wowote wa mikoa yote 34 ya Afghanistan, lakini amesema kundi hilo linaweza kudhibiti kikamilifu nchi hiyo ila uwezekano mwingine bado upo ambapo majeshi ya serikali ya Afghanistan yatajaribu kujiimarisha katika sehemu yanayozidhibiti kwa kulinda miji muhimu ikiwemo Kabul.

Tangu majeshi yanayoongozwa na Marekani yalipoondoka Afghanistan mwezi wa Mei mwaka huu, kundi la Taliban na majeshi ya serikali yalianzisha mapambano makali kugombea udhibiti wa maeneo nchini humo.