Madai kuhusu chanzo cha virusi vya Corona ni kuvuja kutoka maabara ya Wuhan yanaenda kinyume na sayansi
2021-07-23 08:08:38| CRI

Naibu Mkurugenzi wa kamati ya afya ya taifa ya China (NHC) Bw. Zeng Yixin, amesema madai kuwa chanzo cha virusi vya Corona ni kuvuja kutoka kwenye maabara ya Wuhan ni kinyume na sayansi.

Bw. Zeng amesema ameshangazwa kusikia baadhi ya watu wakisema chanzo cha virusi hivyo ni kuvuja kutoka kwenye maabara ya taasisi ya virusi ya Wuhan (WIV), na kusema madai hayo yanapuuza mantiki ya kawaida na yanakwenda kinyume na sayansi.

Mkurugenzi wa usalama wa maabara kwenye taasisi ya virusi ya Wuhan Bw. Yuan Zhiming, amesema tangu maabara ya taasisi hiyo ianzishwe mwaka 2018 hakuna ajali yoyote ya kuvuja kwa virusi iliyotokea.

Bw. Zeng pia amekumbusha kuwa watalaam wa shirika la afya duniani WHO, baada ya kutembelea maabara hiyo walisema “haiwezekani kabisa” kuwa virusi hivyo vilivuja kutoka maabara.