Katibu mkuu wa UM atoa wito wa uongozi wa G20 kwenye harakati za kukabliana na mabadiliko ya tabianchi
2021-07-26 08:28:48| cri

 

 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana ametoa wito wa uongozi wa Kundi la Nchi 20 (G20) kwenye harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Katika taarifa yake kwenye mkutano wa mawaziri wa Kundi hilo kuhusu mazingira, hali ya hewa na nishati, Bw. Guterres amesema, dunia inahitaji ahadi ya wazi kwa nchi zote za Kundi hilo kuhusu lengo la digrii 1.5 ya Mkataba wa Paris, na hakuna njia ya kufikia lengo hilo bila uongozi wa G20.

Zikiwa zimebaki siku chini ya 100 kabla ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika Glasgow, Scotland, Bw. Guterres amewataka viongozi wa Kundi la Nchi 20 na nchi nyingine kuahidi kutimiza kutotoa hewa chafu itakapofika katikati ya karne hii.