Tume ya Uchaguzi ya Myanmar yatangaza kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana
2021-07-27 08:40:59| cri

 

 

Tume ya Uchaguzi nchini Myanmar iliyoundwa upya jana imetangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 mwezi Novemba mwaka jana, kwa kuwa ulikuwa kinyume cha sheria na haki.

Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imesema, ilifanya ukaguzi wa kura zilizopigwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, na kugundua ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi.

Myanmar ilifanya uchaguzi mkuu mwezi Novemba mwaka jana, na chama cha siasa cha Umoja wa Demokrasia wa Kitaifa ulipata zaidi ya nusu ya viti vya bunge. Hata hivyo, Jeshi la nchi hiyo na Chama hicho vilikuwa na mgongano kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu.