Asilimia 80 ya wapiga kura mtandaoni waona suala la kutafuta chanzo ya virusi vya Corona linachochewa kisiasa
2021-07-27 10:41:31| Cri

Kura za maoni zilizokusanywa na jumuiya ya washauri bingwa ya CGTN kwa lugha sita rasmi za Umoja wa Mataifa kwenye mtandao wa Internet hivi karibuni, zimeonyesha kuwa asilimia 80 ya wapiga kura duniani wanaona suala la kutafuta chanzo za virusi vya Corona linachochewa na sababu za kisiasa.

 

Kwa mujibu wa uchambuzi wa maoni hayo, maneno yaliyotokea mara nyingi zaidi kwenye maoni ya wanamtandao ni “shinikizo la kisiasa”, “vikwazo vinavyowekwa na Marekani”, ”kudhibiti maoni kwa vyombo vikuu vya habari” na “kuzuia maendeleo ya China”.

 

Kuna mtumiaji wa mitandao ya kijamii anayetumia lugha ya Kiingereza ameacha maoni yake akisema Shirika la Afya Duniani (WHO) halitakiwi kukubali shinikizo la kisiasa lililowekwa kwenye suala la kutafuta chanzo za virusi vya Corona, ambalo linatumiwa na Marekani kama mkakati wa kuzuia maendeleo ya China. Na mtumiaji wa lugha ya Kifaransa amesema Marekani inataka kuweka vikwazo dhidi ya China kwa kisingizio hicho. Na maoni mengine ya lugha za Kiarabu na Kirusi yamesema nchi za magharibi zinajaribu kuanzisha vita isiyoonekana kutumia suala hilo na umma hautakiwi kudanganywa na wanasiasa.

 

Matokeo ya upigaji kura wa maoni ya wanamtandao wa lugha za Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, Kiarabu, na Kirusi kuhusu kuunga mkono uchunguzi wa chanzo cha COVID-19 katika nchi mbalimbali yanaonesha kuwa asilimia 83 ya watu walipiga kura ya ndiyo katika jukwaa la Twitter, asilimia 79 ya watu walipiga kura za ndiyo kwenye jukwaa la Facebook, na asilimia 93 ya watu walipiga kura ya ndiyo katika jukwaa la Weibo la China.

 

Wakijibu swali kutoka kwa jumuiya ya washauri bingwa ya CGTN, "Je! Unafikiria ni kazi gani ya dharura inatakiwa kufanywa ili kulishinda janga la COVID-19 duniani?", miongoni mwa machaguo matano yakiwemo "kupanua utoaji wa chanjo", "kuimarisha matibabu", " kufuatilia mara moja virusi vinavyotokea ", "kuweka zuio katika maeneo yanayokumbwa na janga hilo na “kuondoa vizuizi vya usafiri”, wanamtandao wengi walichagua "kupanua utoaji wa chanjo", "kuimarisha matibabu", na "kuweka zuio kwenye maeneo ya yanayokumbwa na janga hilo na kuacha kuchagua" kufuatiliwa virusi vinavyotoka mara moja".  

 

Wanamtandao kutoka nchi mbalimbali wamefikia maoni ya pamoja kwa haraka na kwa ufanisi, wakielezea maoni yao kwa lugha tofauti, "Uchunguzi wa chanzo cha virusi vya Corona haudhibiti janga hilo. Hii ni sera ya kisiasa ya Marekani ya kuzuia maendeleo ya China.” "Nadhani kazi muhimu ya sasa ni kuhakikisha ufanisi na usahihi wa chanjo zinazotengenezwa na nchi mbalimbali ili watu waweze kuchagua." Pia wamesisitiza kuwa chanjo ya COVID-19 duniani inapaswa kusimamiwa, na wameitaka China iendelee kutoa chanjo ya bei nafuu na yenye uhakika kwa watu duniani.