China yaitaka Marekani kutoa taarifa za ukweli kuhusu maabara ya baiolojia ya Fort Detrick
2021-07-27 08:34:07| CRI

Vyombo vya habari na wataalamu kutoka nchi mbalimbali wameilaumu Marekani kwa kufanya kazi ya kutafuta chanzo cha virusi vya Corona kuwa ya kisiasa, na kusema kuwa, inapaswa kuchunguza maabara ya baiolojia ya Fort Detrick ya nchini humo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, mbinu ya Marekani ya kisiasa kwa kutumia kazi ya kutafuta chanzo cha virusi imekuwa wazi duniani, na Marekani inapaswa kuonyesha msimamo wa wazi na kuwajibika, kuwaalika wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini humo ili kufanya uchunguzi katika maabara ya Fort Detrick, na kuweka wazi ukweli halisi kwa dunia.