China yaweka mstari wa mwisho kwa uhusiano wake na Marekani
2021-07-27 09:51:32| cri

 

 

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi jana alipokutana na naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Wendy Sherman, ambaye yupo ziarani nchini China, ameweka mstari wa mwisho ili kuhakikisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili unathibitika.

Wang amesisitiza kuwa, Marekani haiwezi kutoa changamoto, kuchafua ama kujaribu kubadili mfumo maalum wa Ujamaa wa China, haiwezi kujaribu kuzuia au kukatisha mchakato wa maendeleo ya China, na pia haiwezi kuharibu mamlaka ya utawala na ukamilifu wa ardhi ya China.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Xie Feng siku hiyo pia amefanya mazungumzo na Sherman, na kusema China inataka Marekani isahihishe makosa yake katika masuala ya chanzo cha virusi vya Corona, Taiwan, Hong Kong, Xinjiang na Bahari ya Kusini, kuacha kuingilia mambo ya ndani ya China na kuharibu maslahi ya China.