China na Marekani zatakiwa kutafuta njia ya kuishi kwa amani kwa pamoja kupitia mazungumzo
2021-07-28 08:35:06| cri

 

 

     Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana amesema, msimamo wa China kuhusu uhusiano wake na Marekani ni wazi kwamba, pande hizo mbili zinapaswa kutafuta njia ya kuishi kwa amani na kunufaishana kupitia mazungumzo.

Amesema kwa nchi kubwa mbili zenye utaratibu tofauti, utamaduni tofauti na vipindi taofauti vya maendeleo, zinapaswa kujenga uhusiano wa kunufaishana na kupata maendeleo ya pamoja.

     Bw. Zhao amesema, nchi hizo mbili zinapaswa kuheshimiana, kushindana kwa haki, na kuishi kwa amani, kwani uhusiano wenye utulivu kati ya nchi hizo mbili utazinufaisha nchi hizo na dunia kwa ujumla.