Mamlaka ya forodha ya China yatangaza mpango wa maendeleo ya miaka 5 ijayo
2021-07-28 08:40:21| CRI

Idara Kuu ya Forodha ya China jana imetangaza mpango wa 14 wa miaka mitano wa maendeleo ya forodha, ambao unazingatia ushirikiano wa kimataifa, na utasukuma mbele maendeleo yenye sifa ya juu ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Mpango huo ni pamoja na sehemu 10 zenye pande tatu, na kuweka wazi malengo halisi ya maendeleo katika ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ujenzi wa maeneo ya biashara huria, afya ya umma katika maeneo ya mpakani, uhifadhi wa hakimiliki za ujuzi, usalama wa baiolojia katika mipaka na mapambano dhidi ya biashara ya magendo.

Mpango huo pia unasema inapaswa kuhimiza kuinua kiwango cha usalama na urahisi wa biashara katika nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kuunga mkono ujenzi wa njia ya usafirishaji wa mizigo kati ya Ulaya na Asia.