Iran yasema nchi za Magharibi hazina uaminifu kwenye mazungumzo kuhusu suala la nyukilia la Iran
2021-07-29 08:42:32| cri

 

 

Kiongozi wa juu zaidi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei jana amesema, nchi za Magharibi ikiwemo Marekani hazina uaminifu kwenye mazungumzo kuhusu suala la nyukilia la Iran.

Akizungumza kwenye mkutano na maofisa wa serikali akiwemo rais Hassan Rouhani, Khamenei amesema kuwa kwenye mazungumzo ya hivi karibuni, Marekani ilishikilia msimamo wake na haikuwa tayari kubadilika katika majadiliano hayo. Amesema, Marekani iliahidi kuondoa vikwazo dhidi ya Iran, lakini kihalisi haikutimiza ahadi yake na haina mpango wa kutimiza ahadi hiyo, bali nchi hiyo inataka kuongeza masharti kwenye makubaliano yaliyofikiwa awali.

Khamenei amesema, serikali ya Iran haipaswi kutegemea nchi za Magharibi kwenye mambo ya ndani.