Asilimia 80 ya watumiaji mtandao waona suala la kutafuta chanzo cha virusi vya Corona linafanyika kisiasa
2021-07-29 08:40:34| CRI

Matokeo ya uchunguzi wa maoni yaliyotolewa na jopo la washauri bingwa la CGTN yameonyesha kuwa, asilimia 80 ya watumiaji mtandao wamesema baadhi ya nchi zinaifanya kazi ya kutafuta chanzo cha virusi vya Corona kuwa suala la kisiasa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana amesema, watumiaji mtandao walioshiriki kwenye uchunguzi huo wanatumia lugha tofauti kueleza maoni ya pamoja, kwamba “uchunguzi wa chanzo cha virusi vya Corona hausaidii katika kudhibiti maambukizi, na unaficha mbinu ya kisiasa ya Marekani kuzuia ustawi wa China”.

Bw. Zhao Lijian amesema, jopo la washauri bingwa la CGTN limefanya uchunguzi huo kwenye mtandao wa Internet kwa kutumia lugha za Kichina, Kiingereza, Kirussia, Kifaransa na Kihispania, na kuonyesha malalamiko ya watu kuhusu Marekani kuifanya kazi ya kutafuta chanzo cha virusi vya Corona kuwa ya kisiasa.