WHO yatakiwa kuchunguza Maabara ya Fort Detrick ya Marekani
2021-07-30 09:00:45| CRI

 

 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limepanga kufanya awamu ya pili ya kutafuta chimbuko la virusi vya Corona, na kusema kuna uwezekano kwamba virusi hivyo vimetoka katika maabara.

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limetoa tahariri ikisema, WHO inapaswa kuchunguza Maabara ya Fort Detrick ya Marekani kutokana na matakwa ya jamii ya kimataifa. Katika hojaji iliyofanywa na CMG, takriban asilimia 80 ya wanamtandao duniani wanaunga mkono kufanya uchunguzi wa chimbuko la virusi vya Corona katika nchi zote zenye mashaka.

Mwanahistoria wa Russia Sergei Latyshev ameandika makala inayoitwa “Je! Maabara ya Fort Detrick ya Marekani ni chimbuko la virusi vya Corona?”, akisema katika suala la kutafuta chimbuko la virusi hivyo, China inaaminika zaidi kuliko Marekani.

Mtoa maoni mashuhuri wa Philippine Herman Laurel pia ameandika makala, akiihimiza WHO kuchunguza Maabara ya Fort Detrick.