Ofisa wa WHO asema utoaji wa chanjo ya virusi wa China wasaidia Afrika kukabiliana na maambukizi ya virusi
2021-07-30 10:37:59| Cri

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani WHO kanda ya Afrika Dkt Matshidiso Moeti amesema hadi sasa watu milioni 21 tu barani Afrika wamepewa dozi kamili ya chanjo ya COVID-19, na kuzihimiza nchi tajiri kusambaza chanjo nyingi zaidi kwa nchi za Afrika.

Dkt Moeti amesema hadi sasa Afrika bado inahitaji dozi zaidi ya milioni 700 za virusi vya Corona, ili kutimiza lengo la kuchanja asilimia 30 ya watu wote kabla ya mwishoni mwa mwaka huu. Mpango wa ugavi wa COVAX umefikia makubaliano na makampuni ya Sinopharm na Sinovac ya China kutoa dozi milioni 110 za chanjo kwa nchi zenye kipato cha chini duniani, na dozi milioni 32.5 kati ya hizo zitasafirishwa barani Afrika.

Pia ameonya kuwa bara la Afrika linaendelea kukabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi, idara za afya za nchi mbalimbali za Afrika zinatakiwa kuendelea na hatua mbalimbali za zuio.