Marais wa China na Sierra Leone wapeana salamu za pongezi katika kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi
2021-07-30 08:56:21| cri

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Sierra Leone, Julius Maada Bio jana wamepeana salamu za pongezi katika kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Rais Xi amesema, katika nusu karne tangu kuanzishwa kwa uhusiano huo, nchi hizo mbili zimeelewana na kusaidiana katika masuala muhimu yanayohusu maslahi makuu na ufuatiliaji ya kila upande. Amesisitiza kuwa anazingatia sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Sierra Leone, na anapenda kushirikiana na rais Bio kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote ambayo yatanufaisha watu wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, rais Bio amesema ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umepata mafanikio makubwa, na Sierra Leone inatarajia kushirikiana na China kuimarisha zaidi urafiki wa jadi na ushirikiano kati yao katika sekta mbalimbali.