Bach awapongeza wanamichezo wa China kwa mafanikio mazuri katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo
2021-07-30 09:01:28| CRI

 

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) Bw. Thomas Bach amewapongeza wanamichezo wa China kwa mafanikio yao katika michezo hiyo.

Bw. Bach amesema hayo alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Utangazaji cha Michezo ya Olimpiki ya Tokyo (IBC). Amesema mafanikio mazuri waliyopata wanamichezo wa China katika michezo mbalimbali yameifanya dunia ione China yenye maendeleo mazuri na ya kasi. Pia amemshukuru rais Xi Jinping wa China kwa pendekezo lake la kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, na kuwahamasisha Wachina milioni 300 kushiriki katika michezo hiyo.

Pia amesema IOC ina uhusiano wa karibu na CMG, na kuamini kuwa Michezo ya Olimpiki ya Kimataifa itakuwa alama muhimu katika ushirikiano kati ya pande hizo mbili.