Awamu ya pili ya mpango wa kutafuta chanzo cha COVID-19 haujakubaliwa na wanachama wote WHO
2021-07-30 10:58:08| Cri

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Zhao Lijian jana alisema kuwa awamu ya pili ya mpango wa Shirika la Afya Duniani kuhusu kutafuta chanzo cha COVID-19 uliotangazwa na sekretarieti ya shirika hilo haukuidhinishwa na nchi zote wanachama wa shirika hilo.

Bw. Zhao alisema WHO inaongozwa na nchi wanachama na sekretariti yake imetoa rasimu ya mpango ili kujadiliwa na nchi zote wanachama ambao wana haki ya kuurekebisha. Jukumu la sekretarieti ni kutoa urahisi kwa nchi wanachama kufanya majadiliano na kufikia makubaliano, lakini haina haki ya kufanya uamuzi yenyewe.