Myanmar kufanya uchaguzi mkuu katika nusu ya pili ya mwaka 2023
2021-08-02 09:12:48| cri

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Ulinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza jipya la Utawala la Taifa Bw. Min Aung Hlaing amesema kuwa Myanmar inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mpya katika nusu ya pili ya mwaka 2023 ambayo itakuwa Agosti, baada ya kufanya maandalizi kwa miezi sita.

Akilitangazia taifa kupitia televisheni, Kamanda Min Aung Hlaing pia aliahidi kufanya uchaguzi mkuu wa vyama vingi, akisisitiza haja ya kuweka mazingira ya kufanya uchaguzi mkuu ulio huru na wa haki wa vyama vingi.

Pia aliahidi kushirikiana na Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN).