Rais wa Misri na waziri wa mambo ya nje wa Algeria wajadili uhusiano wa pande mbili na masuala ya kikanda
2021-08-02 09:09:26| cri

Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri na waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Ramtane Lamamra wamefanya mazungumzo jana juu ya uhusiano wa pande mbili na masuala kadhaa ya kikanda mjini Cairo.

Kwenye mazungumzo yao, rais Sisi amesisitiza kuwa Misri inataka kuendeleza ushirikiano na Algeria kwenye sekta mbalimbali, kwa namna ya kuonyesha uhusiano wa kindugu kati ya wananchi wa pande mbili. Kwa upande wake Bw. Lamamra amesema nchi yake inapenda kuimarisha ushirikiano na Misri na kupanua maeneo mapya ya ushirkiano.

Pia wameeleza umuhimu wa kuunga mkono uratibu wa kisiasa na kuhimiza usalama na kubadilishana taarifa kwenye mapambano dhidi ya ugaidi na itikadi kali. Mbali na hayo, wamebadilishana maoni juu ya masuala ya kikanda hasa hali ya Libya, na kusisitiza haja ya kuunga mkono idara za serikali ya Libya na juhudi zinazofanywa kwa ajili ya kutimiza usalama na utulivu na kulinda umoja na mamlaka ya nchi.