Afisa wa UNRWA aonya uhaba wa malighafi wachelewesha ukarabati huko Gaza
2021-08-02 08:52:28| Cri

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina la Umoja wa Mataifa katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) limeonya juu ya uhaba wa malighafi katika mpango wa kuanza ukarabati wa Ukanda wa Gaza.

Akitoa taarifa kwenye mkutano na wanahabari, Mkurugenzi wa UNRWA huko Gaza Sam Rose amesema kuwa, ukosefu wa malighafi unatokana na kufungwa kwa njia ya kipekee ya kibiashara kati ya Gaza na Israel.”

Jumapili Israeli ilianza kulegeza vizuizi ambavyo viliwekwa katika Ukanda wa Gaza tangu duru ya mwisho ya mvutano ambayo ilidumu kwa siku 11 na kumalizika Mei 21.

Mkuu wa shughuli za uratibu wa serikali kwenye sehemu hiyo Ghassan Alian amesema kwenye taarifa kuwa itawezekana kupeleka vifaa na bidhaa huko Gaza, ikiwa ni pamoja na vifaa vya miradi inayofadhiliwa na jamii ya kimataifa vikiwemo chakula, maji, dawa na uvuvi. Pia amesisitiza mahitaji ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa kuvuka kituo cha biashara kati ya Palestina na Israeli ili kuunga mkono mchakato wa ukarabati huko Gaza.