Baraza kuu la Umoja wa Mataifa laanzisha Jukwaa la kudumu kwa watu wenye asili ya Afrika
2021-08-03 09:22:24| cri

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa jana lilipitisha azimio la kuanzisha Jukwaa la kudumu kwa watu wenye asili ya Afrika, likiwa kama utaratibu na chombo cha mashauriano kwenye Baraza la Haki za Binadamu.

Kazi za jukwaa hilo ni pamoja na kuhimiza watu wenye asili ya Afrika wawe na haki sawa katika kujiunga na mambo ya siasa, uchumi na jamii bila ya ubaguzi wowote, na kuhakikisha wananufaika na haki zote za binadamu kwa usawa.

Mbali na hayo, jukwaa hilo litawasilisha ushauri na mapendekezo ya kitaalamu kwa Baraza la Haki za Binadamu na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia changamoto za ubaguzi wa rangi,  chuki dhidi ya wageni na nyingine zisizovumilika. Pia jukwaa hilo litashughulikia kujadili azimio la Umoja wa Mataifa juu ya kuhimiza, kulinda na kuheshimu haki za binadamu kwa watu wenye asili ya Afrika.