Iran yaonya kuwa itajibu vikali na haraka juu ya tukio la meli ya mafuta
2021-08-03 09:10:06| cri

Wizara ya Mambo ya nje ya Iran imetupilia mbali tuhuma za Uingereza na Marekani kuhusu ripoti ya ndege isiyo na rubani kushambulia meli ya mafuta inayosimamiwa na Israel kaskazini mwa Bahari ya Arabia, na kuonya kwamba itajibu vikali na haraka tuhuma zozote zile.

Msemaji wa wizara hiyo Bw. Saeed Khatibzadeh amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasita hata kidogo kulinda usalama wake na maslahi ya kitaifa.