Marekani yawataka wanadiplomasia 24 wa Russia waondoke kabla ya Septemba 3
2021-08-03 09:09:00| cri

Balozi wa Russia nchini Marekani Anatoly Antonov amesema Marekani imewataka wanadiplomasia 24 wa Russia waondoke nchini humo kabla ya tarehe 3, Septemba kwa sababu ya viza zao kumaliza muda.

Bw. Antonov amesema mwezi Disemba mwaka jana Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani bila kutoa taarifa iliweka ukomo wa miaka mitatu kwa wafanyakazi wa Russia kufanya kazi nchini Marekani, ambapo kwa ufahamu wake anasema hajawahi kuona ikifanyika katika nchi nyingine.

Kauli hiyo ya balozi wa Russia imekuja siku mbili baada ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kusema kuwa iliwafukuza wafanyakazi wenyeji 182 na makumi ya wakandarasi katika vituo vya kidiplomasia vya Marekani nchini Russia kufuatia agizo la Russia.