Timu huru yasema nchi tajiri bado ziko mbali kufikia malengo ya uchangiaji wa chanjo ya COVID-19
2021-08-04 08:52:08| cri

Ripoti ya hivi karibuni ya Al Jazeera ambayo iliinukuu timu huru inayofuatilia mwitikio wa dunia juu ya janga la COVID-19 imesema kwamba nchi tajiri hazijachangia vya kutosha chanjo za COVID-19 kwa nchi zinazoendelea.

Mwezi Mei, Timu Huru ya Kujiandaa na Kuitikia Janga (IPPPR) iliyoanzishwa na Shirika la Afya Duniani WHO, ilizitaka nchi zenye kipato cha juu kutoa dozi bilioni moja za chanjo kwa nchi zenye kipato cha chini na cha kati ifikapo mwezi Septemba, na bilioni moja nyingine ifikapo katikati ya mwaka 2022. Kwa mujibu wa IPPPR, kuna haja kubwa ya kubadilisha njia za chanjo na matibabu.