Wanachama wengi wa WHO wakubali kuacha kulifanya suala la kutafuta chanzo cha virusi kuwa la kisiasa
2021-08-04 08:51:12| cri

Mkurugenzi mtendaji wa mradi wa dharura wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Michael Ryan amesema nchi wanachama wengi wa WHO wanakubali kuacha kulifanya suala la kutafuta chanzo cha virusi vya Corona kuwa la kisiasa, ili kuweka msingi mzuri kwa kazi hiyo.

Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika tarehe 30 mwezi Julai, Ryan amesema wanachama wengi ikiwemo China wanajitahidi kutafuta njia ya kuhimiza mchakato wa utafiti wa kutafuta chanzo cha virusi vya Corona. Pia ameipongeza China kwa kutoa mchango katika kutafuta chanzo cha virusi.

Amesisitiza kuwa kazi inayofuata katika kutafuta chanzo cha virusi inapaswa kuendelea kufuata mwongozo wa sayansi, na Shirika la Afya Duniani linataka jamii ya kimataifa iuunge mkono ushirikiano kwenye mchakato huo, na kutaka kazi hiyo iendelee kufanyika kote duniani.