Mlipuko mkubwa watokea kwenye makazi ya waziri wa ulinzi wa Afghanistan
2021-08-04 09:45:16| Cri

Bomu lenye nguvu kubwa limelipuka mjini Kabul jana Jumanne saa mbili usiku kwa saa za Afghanistan, na baadaye kufuatia milio ya risasi.

Msemaji wa polisi ya Kabul Bashir Mujahid amesema mlipuko huo ulitokea katika wilaya ya 10 ya kipolisi, baada ya wanamgambo wasiojulikana kuanza kulipua bomu lililotegwa kwenye gari karibu na makaazi ya Waziri wa Ulinzi wa Afghanistan Bismillah Khan Mohammadi, ambapo mlipuko huo ulifuatiwa na milio ya risasi. Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya mlipuko huo washambuliaji waliingia kwenye eneo la makaazi ya waziri na kuendelea kufyatua risasi.

Bw. Mujahid amesema taarifa zaidi zitatolewa baada ya kufanyika kwa uchunguzi