Idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona yazidi milioni 200 kote duniani
2021-08-05 09:03:38| cri

Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zimeonyesha kuwa hadi jana idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona imezidi milioni 200 kote duniani.

Takwimu zimeonyesha kuwa hadi jana mchana kwa saa za Marekani, idadi ya jumla ya watu walioambukizwa virusi imefikia 200,014,602 kote duniani, na idadi ya vifo imefikia 4,252,873. Marekani, India na Brazil ni nchi tatu zenye idadi kubwa zaidi ya watu waliothibitishwa duniani.

Mkuu wa taasisi ya mzio na magonjwa ya kuambukiza ya Marekani Bw. Anthony Fauci jana alisema, idadi ya watu walioambukizwa virusi vipya vya Delta inaweza kuongezeka mara dufu na kufikia laki mbili kwa siku katika majira ya mpukutiko nchini Marekani.