China kutoa dozi bilioni 2 za COVID-19 duniani mwaka huu
2021-08-06 09:22:46| Cri

China itajitahidi kutoa dozi bilioni 2 za COVID-19 duniani mwaka huu na kutoa dola za kimarekani milioni 100 kwenye mpango wa COVAX.

Rais Xi Jinping wa China amesema hayo kwenye risala ya maandishi aliyoitoa kwenye Baraza la Kimataifa kuhusu ushirikiano wa chanjo ya COVID-19

Amesema dola milioni 100 za kimarekani kwa ajili ya mpango wa COVAX zitatumiwa katika kusambaza chanjo kwa nchi zinazoendelea, akiongeza kuwa China itafanya bidii kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na janga la COVID-19.

Rais Xi amesisitiza kuwa China inajitahidi kujenga jumuiya yenye afya duniani kwa watu wote na pia imetoa chanjo duniani, haswa kwa nchi zinazoendelea. Aidha amesema China inafanya ushirikiano katika uzalishaji, hatua ambayo imeonesha dhana ya kuifanya chanjo iwe bidhaa ya umma duniani.