Mamlaka za China zapongeza wanariadha kutokana na mafanikio waliyopata katika Michezo ya Olimpiki
2021-08-09 08:37:05| CRI

Mamlaka kuu za China zimetuma barua ya pongezi kwa ujumbe wa Olimpiki wa China kutokana na mafanikio waliyoyapata katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo.

Barua hiyo iliyotolewa kwa pamoja na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Baraza la Serikali la China, inasema “Mmeleta sifa kubwa kwa taifa na watu wenu, na tunatoa pongezi nyingi kwenu. Mmekabiliana na changmoto kubwa zinazotokana na janga la COVID-19, na kukamilisha vizuri jukumu letu.”Barua hiyo pia imesema wanariadha hao wa China wameonyesha ustadi mkubwa na morali wa hali ya juu, ambavyo vinatafsiri kidhahiri roho ya Olimpiki na moyo wa uanamichezo wa China.

Kamati kuu ya CPC na Baraza la Serikali la China pia wametoa wito kwa wanariadha kutobweteka na kuendelea na juhudi ili kuongeza nguvu zaidi michezo ya China na uwezo wao wa kuleta sifa kubwa zaidi kwa taifa lao.

Katika Michezo ya Olimpiki iliyofungwa jana, China ilichukua nafasi ya pili kwa idadi ya medali, ambazo ni 38 za dhahabu, 32 za fedha na 18 za shaba.