China yapinga kithabiti Marekani kusaini hati ya makubaliano yanayohusu Hongkong
2021-08-09 08:37:33| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Hua Chunying amesema China inapinga kithabiti Marekani kusaini hati ya makubaliano yanayohusu Hongkong, na imetoa malalamiko makali kwa upande wa Marekani.

Bi. Hua Chunying amesema hati hiyo ya makubaliano iliyosainiwa na rais wa Marekani inakashifu na kushambulia Sheria ya Jamhuri ya Watu wa China kuhusu Kulinda Usalama wa Taifa Mkoani Hongkong na sera ya China kwa Hongkong, ambayo ni kitendo kingine cha Marekani kuingilia mambo ya Hongkong ya China.

Bi. Hua amesema kupitishwa na kutekelezwa kwa sheria hiyo kumeboresha utawala wa sheria mkoani Hongkong, kurejesha usalama na utulivu mkoani humo, na kuhakikisha haki halali na maslahi ya wakazi wa Hongkong.

Ofisi ya Masuala ya Hongkong na Macao ya Baraza la Serikali ya China jana jumapili pia ilitoa tamko rasmi la kupinga na kulaani uingiliaji wa Marekani katika masuala ya Hongkong, ambayo ni mambo ya ndani ya China.