China yaamua kurejesha balozi wake nchini Lithuania
2021-08-10 22:52:51| Cri

Hivi karibuni Serikali ya Lithuania imetangaza kuruhusu mamlaka ya Taiwan kuanzisha ofisi yake nchini humo kwa jina la “Taiwan”, bila ya kujali malalamiko ya China. Kitendo hiki kimekiuka waziwazi taarifa ya pamoja kuhusu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, na kuharibu vibaya mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa China. Serikali ya China inakipinga kithabiti, na kuamua kurejesha balozi wake  nchini Lithuania.

China inasisitiza kuwa, kuna China moja tu duniani, na serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee yenye uhalali wa kisheria inayowakilisha China. Pia inaiharakisha Lithuania kujirekebisha uamuzi wake usiofaa mara moja, kuchukua hatua zenye ufanisi kuondoa athari mbaya, na kutokwenda mbali katika njia yenye makosa.