Rais wa Zambia akutana na timu ya uangalizi ya Umoja wa Afrika kabla ya uchaguzi kufanyika
2021-08-10 14:33:40| CRI

Rais Edgar Lungu wa Zambia jana amekutana na timu ya uangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika kabla ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 12 mwezi huu.

Rais Lungu amefanya mazungumzo na timu hiyo inayoongozwa na rais wa zamani wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma kwenye ikulu ya Zambia. Kwenye mazungumzo yao, rais Lungu amehimiza timu hiyo itekeleze majukumu yake kwa makini na kuchunguza vitendo vya baadhi ya vyama vya upinzani. Kwa upande wake, Mkuu wa timu hiyo Bw. Bai Koroma amesema, waangalizi 30 watafanya kazi kwenye mikoa 10 nchini humo, ili kuhakikisha amani, usalama na demokrasia kwenye kipindi cha uchaguzi.