Utafiti waonesha kuwa kulungu wengi wenye mkia mweupe (Whitetail Deer) waliwahi kuambukizwa COVID-19
2021-08-10 22:52:14| Cri

Tovuti ya Gazeti la Uingereza Nature hivi karibuni ilitoa ripoti kuwa, utafiti kuhusu sampuli za damu za kulungu wenye mkia mweupe  (Whitetail Deer) wanaoishi katika kaskazini mashariki nchini Marekani ambao ulifanywa na watafiti wa Wizara ya Kilimo ya Marekani umeonesha kuwa, theluthi moja ya kulungu hao waligunduliwa kuwa na kingamwili ya COVID-19, hali ambayo imeonesha kuwa waliwahi kuambukizwa virusi hivyo.

Wataalamu wengine bado hawajatoa maelezo juu ya ripoti hiyo.

Utafiti huo ulifanyika juu ya sampuli 385 za damu za kulungu wenye mkia mweupe ambazo zilikusanywa kati ya Januari hadi Machi mwaka 2021, na kuonesha kuwa asilimia 40 ya sambuli ziligunduliwa kuwa na kinga mwili dhidi ya COVID-19, lakini kulungu hao hawakuonesha dalili ya ugonjwa huo. Habari zinasema kuwa matokeo ya utafiti juu ya sampuli zilizokusanywa mwaka 2020 na 2021 yameonesha kuwa, theluthi ya kulungu hao waligunduliwa kuwa na kinga mwili dhidi ya COVID-19.

Ripoti hiyo pia inasema, swali kubwa kwa sasa ni kuwa kulungu hao waliambukizwa virusi kwa njia gani. Mwanasanyansi wa virusi wa Chuo Kikuu cha Saskatchewan cha Canada Arinjay Banerjee amesema, ikiwa kulungu hawa waliambukizwa kutoka chanzo sawa, wanyama wengine wanaweza pia kuwasiliana na chanzo hiki cha maambukizi.