Korea Kusini yasema Korea Kaskazini imekataa kupokea simu ya mawasiliano kati ya nchi hizo mbili
2021-08-11 09:33:02| CRI

Wizara ya Umoja ya Korea Kusini imesema, Korea Kaskazini haikupokea simu ya kawaida kutoka Korea Kusini kupitia njia ya mawasiliano ya kijeshi na ofisi ya mawasiliano kati ya nchi hizo mbili, na upande wa Korea Kusini utafuatilia kwa makini hali husika.

Uchambuzi unaonesha kuwa uamuzi huo wa Korea Kaskazini ni kitendo cha kuonyesha kutoridhishwa na luteka ya pamoja iliyofanywa na Korea Kusini na Marekani.

Shirika la habari la Korea Kusini YNA limesema, leo asubuhi serikali ya Korea Kusini itajaribu tena kuupigia simu upande wa Korea Kaskazini.