Wamarekani wengi watumia mtandao wa Twitter wakisema waliambukizwa COVID-19 mapema sana
2021-08-11 10:39:22| cri

Wamarekani zaidi ya 1000 walitumia mtandao wa kijamii wa Twitter wakisema kuwa wao binafsi, familia zao au marafiki zao waliambukizwa virusi vya Corona kabla ya Desemba mwaka 2019, huku watu zaidi ya 100 waliotaja majina yao halisi wameandika dalili za ugonjwa zinazofanana sana na dalili za COVID-19.

Mkazi mmoja wa Washington anayeitwa Jamie Kettenhofen aliandika kwenye Twitter kuwa mke wake na daktari wanaaminika kwamba aliambukizwa COVID-19 tarehe Mosi mwezi Oktoba mwaka 2019, na alitengwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku 10. Na walifanya vipimo mara nyingine na kushindwa kuthibitisha ana virusi vya aina gani au homa gani ya mapafu.

James Krutocks naye aliandika kwamba pengine aliambukizwa mwezi Novemba au Desemba mwaka 2019, na alienda kwenye kitengo cha dharura kwa kuwa alikuwa na matatizo ya mapafu na alishindwa kupumua bila ya msaada wa oksijeni.

Mwanamke mwingine aitwaye Kelsey amesema kwenye Twitter tarehe 11 Desemba mwaka 2020 kwamba mtoto wake alikuwa na tatizo la kupumua na homa ya mapafu mwezi Desemba mwaka 2019. Sampuli ya damu yake ilionyesha ana kingamwili ya COVID-19, Sasa anaamini kuwa aliambukizwa na virusi vya Corona wakati ule.

Takwimu zinaonyesha kuwa, watumiaji hawa wa Twitter wametoka sehemu mbalimbali duniani, miongoni mwao asilimia 75 wanatoka Marekani, na wengine kutoka Ulaya, na Amerika ya Kusini.

Hadi sasa, kuna ushahidi mwingi unaoonyesha kuwa, virusi vya Corona huenda viligunduliwa katika sehemu nyingi duniani kabla ya mwisho wa mwaka 2019.