Baraza la Seneti la Marekani laidhinisha muswada wa ujenzi wa miundombinu wenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 1.2
2021-08-11 09:43:33| cri

Baraza la Seneti la Marekani jana lilipitisha muswada wa ujenzi wa miundombinu wenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 1.2 kwa kura 69 za ndio, baada ya majadiliano makali ya miezi kadhaa kati ya wabunge wa vyama vya Democratic na Republican.

Kabla ya kura hiyo, kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Bw. Chuck Schumer alisema, hiyo ni hatua iliyosubiriwa kwa muda mrefu ili kufufua miundombinu ya nchi inayoharibika, na kuongeza kuwa ni fedha nyingi zilizowahi kutolewa kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu katika miongo kadhaa.