Mamlaka ya Mto Zambezi yadumisha mgao wa maji kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa Zimbabwe na Zambia
2021-08-11 09:15:55| CRI

Mamlaka ya Mto Zambezi (ZRA) itaendelea kudumisha mgao wa mita za ujazo bilioni 42 za maji kwa ajili ya Zimbabwe na Zambia kuzalisha umeme kwenye bwawa la Kariba.

Mamlaka hiyo iliyo chini ya nchi hizo mbili kwa pamoja imepewa jukumu la kusimamia maendeleo ya kiuchumi, viwanda na kijamii kwa Zimbabwe na Zambia, kwa kutumia kadiri iwezekanavyo manufaa yanayotokana na maji ya mto Zambezi, kwa kuzalisha umeme na kwa mambo mengine ambayo nchi hizo mbili zinaweza kuamua.

Mwezi Juni ZRA ilitangaza ongezeko la mgao wa matumizi ya maji kwa mita za ujazo bilioni 12, kwa ajili ya uzalishaji wa umeme kwa makampuni ya Umeme ya Zambia na Zimbabwe, mgao utakaoendelea hadi mwishoni mwa mwaka huu

Kaimu ofisa mkuu mtendaji wa ZRA Bw. Edward Kabwe, amesema maji ya Ziwa Kariba yanazidi kupungua, na hadi kufikia Agosti 9 kimo cha maji kilikuwa meta 6.5 juu ya kiwango cha chini cha kuwezesha operesheni (MOL) ambacho ni mita 475.50.