China yatoa waraka mweupe kuhusu maendeleo ya haki za binadamu kupitia mafanikio ya jamii yenye maisha bora
2021-08-12 14:43:59| CRI

China imetoa waraka mweupe kufafanua kuhusu jinsi kutimiza ujenzi wa jamii yenye maisha bora kunavyowakilisha maendeleo ya kina katika kuhakikisha haki za binadamu kwa wote nchini China, na mchango mpya kwa dunia katika masuala ya haki za binadamu.

Waraka huo, “Kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote: Hatua nyingine kubwa kwa haki za binadamu nchini China,” umetolewa leo na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China.

Waraka huo unasema, chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), watu wa China wamemaliza mageuzi ya kihistoria katika kuondokana na umasikini mpaka kuwa na uhakika wa chakula na mavazi, maisha mazuri, na kufikia ustawi wa kati.

Waraka huo umegusa maeneo matano, ambayo ni kutimiza kujenga jamii yenye maisha bora na kuendeleza haki za binadamu, kuondokana na umasikini uliokithiri na kuhakikisha haki ya kuwa na maisha bora, kuboresha haki za binadamu na maendeleo na kutimiza haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni, kulinda haki za raia na siasa kisheria na kiuongozi, na kuboresha usawa wa kijamii na ulinzi wa haki za makundi maalum.