Tembo 57 wauzwa kwa mnada Namibia
2021-08-12 09:16:13| cri

Wizara ya Mazingira, Misitu na Utalii ya Namibia imesema itawauza tembo 57 kwa mnada. Msemaji wa wizara hiyo Romeo Muyunda amesema kati ya tembo hao, 42 watauzwa nchi za nje na wengine 15 watauzwa nchini. Anasema lengo la mnada huo ni kudhibiti idadi ya tembo kwenye eneo maalum na kupunguza migongano kati ya binadamu na tembo. Na pesa zitakazopatikana kwenye mnada zitatumika kwa uhifadhi wa wanyamapori nchini Namibia na usimamizi wa migongano kati ya binadamu na tembo.

Kazi ya kuwasaka tembo hao itaanza mwezi huu na itatekelezwa na shirika la uendeshaji wa uwindaji lililosajiliwa chini ya usimamizi wa wizara ya mazingira.

Kwa mujibu wa idadi rasmi, idadi ya tembo nchini Namibia imeongezeka hadi karibu elfu 24 mwaka 2019 kutoka zaidi ya 7,500 wa mwaka 1995.