China yaihimiza Marekani kuacha kutoa ishara za kosa kwa wafarakanishaji wa Taiwan
2021-08-12 09:01:01| CRI

China imeitaka Marekani ifuate kanuni ya China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, kushughulikia kwa hatua mwafaka masuala yanayohusu Taiwan na kuacha kutoa ishara za makosa kwa wafarakanishaji wa Taiwan.

Msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China Bw. Ma Xiaoguang, ametoa tamko hilo kufuatia Marekani kutangaza nia ya kuimarisha nguvu ya kitisho ya kikanda katika Mlango Bahari wa Taiwan.

Bw. Ma amesema suala la Taiwan ni suala la ndani la China lisiloruhusu uingiliaji wa nje.

Msemaji huyo amesema ni jukumu la pamoja la watu wa China, wakiwemo wazalendo wa Taiwan, kulinda mamlaka ya taifa na ukamilifu wa ardhi ya China. Pia ameonya kuwa kama wafarakanishaji wa Taiwan wakithubutu kufanya uchokozi, “serikali ya China ina haki ya kuchukua hatua zozote za lazima ili kuwazuia.”