Somalia yapata dola za kimarekani milioni 26 kwa ajili ya mwitikio wa kibinadamu
2021-08-12 09:01:26| CRI

Mfuko wa Kibinadamu wa Somalia (SHF), utaratibu unaoshirikisha wahisani wengi nchini humo ambao unatoa fedha kwa ajili ya uingiliaji wa dharura wa kuokoa maisha, umehakikisha utoaji wa dola za kimarekani milioni 26 kwa ajili ya mwitikio wa kibinadamu nchini humo.

Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA, inayosimamia mfuko huo, imesema fedha hizo zitatumika kwenye maeneo yanayokabiliwa na ukosefu mkubwa wa maji kutokana na ukame uliodumu muda mrefu, pamoja na maeneo ya kusini na kati ya Somalia yaliyoathiriwa na mafuriko.

OCHA pia imetahadharisha kuhusu kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu nchini Somalia wakati mashirika ya kibinadamu yanakabiliwa ukosefu mkubwa zaidi wa fedha katika miaka sita iliyopita.

Kwa mujibu wa OCHA, karibu theluthi mbili ya fedha hizo zitatumiwa kwenye shughuli za kipaumbele kama vile usalama wa chakula, huduma za afya, lishe na maji, na huduma za usafi.