China yaitaka Lithuania kuheshimu ahadi yake ya kuwepo kwa China moja
2021-08-12 14:43:29| CRI

China imeitaka Lithuania kuheshimu ahadi yake ya kuwepo kwa China moja, na kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Hayo yamesemwa jana na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying hapa Beijing alipokutana na wanahabari.

Akizungumzia majibu ya Lithuania na Umoja wa Ulaya kuhusu uamuzi wa China, Hua amesema maana ya sera ya kuwepo kwa China moja haipaswi kupotoshwa, na kuongeza kuwa watu wa China hawawezi kuruhusu kitendo cha mahusiano rasmi na mamlaka za Taiwan, na hata kuwafadhili wanaotaka “Uhuru wa Taiwan” huku wakishikilia sera ya kuwepo kwa China moja kwa maneno bila matendo.

Amesema Lithuania haitakiwi kuelewa vibaya msimamo wa China wa kulinda nchi na mamlaka yake na ukamilifu wa ardhi, na kushikilia kikamilifu ahadi yake ya kusuata msimamo wa China moja.