WHO yaongeza majaribio kwa dawa 3 mpya
2021-08-12 09:44:51| cri

 

 

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Tedros Ghebreyesus ametangaza kipindi kingine cha mpango wa majaribio ya dawa dunani unaojulikana kama Solidarity PLUS.

Habari zinasema, kwenye kipindi hicho kijacho, WHO itaongeza majaribio matatu mapya ya dawa za artesunate, Imatinib na infliximab kwa ajili ya kutibu magonjwa ya malaria, saratani na matatizo ya mfumo wa kinga. Majaribio hayo yatafanyika katika hospitali zaidi 600 ya nchi 52 duniani.