Wizara ya mambo ya nje ya China yahimiza nchi husika kuheshimu mamlaka ya kisheria ya China
2021-08-13 14:33:01| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amezitaka nchi husika kufuata utawala wa sheria, kuheshimu mamlaka ya kisheria ya China na kuacha kutoa kauli zisizowajibika.

Bibi Hua amesema, China inalaani vikali kitendo cha Canada kushirikiana na baadhi ya nchi kutozingatia hali halisi na kuingilia kati mamlaka ya utekelezaji wa sheria ya China.

Habari zinasema, raia wa Canada Michael Spavor alihukumiwa kifungo cha miaka 11 jela kwa kosa la kufanya ujasusi nchini China, na raia mwengine wa Canada Robert Lloyd Schellenberg alipewa adhabu ya kifo kwa kosa la kuingiza dawa za kulevya zaidi ya kilogram 222 nchini China.