Wizara ya mambo ya nje ya China yahimiza bunge la Marekani kuacha kutoa ishara za makosa kwa wafarakanishaji wa Taiwan
2021-08-13 11:03:57| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi Hua Chunying amesema, kitendo cha baraza la chini la bunge la Marekani kupitisha mswada kuhusu Taiwan kushiriki katika mkutano wa Shirika la afya duniani WHO ni mchezo wa kisiasa wa wanasiasa wachache wanaoipinga China. Mswada huu umekiuka vibaya kanuni ya uwepo wa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, na kukiuka vibaya sheria za kimataifa na kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa na kuingilia kati mambo ya ndani ya China. China inapinga kithabiti kitendo hicho cha bunge la Marekani.

Agosti 6, baraza la chini la bunge la Marekani lilijadili na kupitisha mswada kuhusu kumtaka waziri wa mambo ya nje wa Marekani kutunga mkakati kuiwezesha Taiwan kupewa hadhi ya mwangalizi wa Shirika la WHO, katika hali ambayo wabunge wachache walikuwepo.

Bi. Hua amesema kwa mujibu wa azimio husika lililotolewa na Umoja wa Mataifa na WHO, eneo la Taiwan la China kushiriki kwenye shughuli za WHO kunatakiwa kufuata kanuni ya uwepo wa China moja. Serikali ya China inafuatilia sana maslahi ya ndugu wa Taiwan, huku ikitoa mpango mzuri kuhusu eneo hilo kushiriki kwenye mambo ya afya ya dunia katika msingi wa uwepo wa China moja.